Spika wa Bunge, Anne Makinda |
Maombi hayo yalifanyika katika mji wa Namgongo nchini Uganda yakiwa na lengo la kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa mwenye heri na hatimaye mtakatifu kulingana na na imani ya dhehebu la kikatoliki.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, maombi hayo maalum hufanyika Juni Mosi kila mwaka kwa mfululizo wa siku saba.
Makamu wa Rais wa Uganda, Edward Ssekandi, ambaye alimwakilisha Rais Yoweri Kaguta Mseven alisema mwalimu Nyerere katika maisha yake alikuwa mtetezi wa haki za wanyonge na kupigania uhuru wa Mwafrika.
Alisema Mwalimu Nyerere alijipatia sifa ndani na nje ya nchi yake na kwamba kamwe wananchi wa Uganda hawawezi kumsahau kwa ajili ya vita vya ukombozi wa nchi yao vya mwaka 1978 hadi 1979.
Viongozi wengine walioshiriki ibada hiyo ni Waziri Mkuu Mstaafu, John Samwel Malecela, Mama Maria Nyerere na watoto wake watatu, akiwamo Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Charles Makongoro Nyerere.
0 comments:
Post a Comment